Nairobi: Nyanda za malisho zatajwa kuwa suluhu kwa usalama wa chakula na tabianchi Afrika

Kwa muda mrefu maeneo ya nyanda za malisho yamekuwa yakitazamwa kama yaliotengwa na yasio na umuhimu, licha ya kuwa na mifumo ikolojia muhimu na chanzo cha riziki kwa takriban watu bilioni mbili duniani, Pamoja na kuhifadhi theluthi moja ya hewa ya kaboni duniani.

Lakini sasa wadau wa mazingira, watunga sera, watafiti, wataalam na wawakilishi kutoka jamii za wafugaji baranai Afrika sasa wanatoa wito wa maeneo ya nyanda za malisho na jamii za wafugaji kutambuliwa.

Katika kongamano la siku mbili lililofanyika jijini Nairobi nchini kenya, kuhusu mustakabali wa nyanda za malisho na jamii za wafugaji, Dkt Eliane Ubalijoro, mkurugenzi mtendaji wa CIFOR-ICRAF, alisema…